Chama cha ACT-Wazalendo kinapenda kualika vyombo vya habari katika Ufunguzi wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kinachotarajiwa kufanyika kesho Oktoba 31,2021 saa 5.30 asubuhi katika Ukumbi wa Hotel ya Land Mark Dar Salaam.
Kikao hicho kitatanguliwa na hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Zuber Kabwe ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ukiwamo mwenendo wa kisiasa hapa nchini.
Halmashauri Kuu ya Chama Taifa ni kikao cha pili kwa ukubwa baada ya Mkutano Mkuu Taifa.
Waandishi wote mnakaribishwa katika tukio hili muhimu.
Imetolewa na:
Arodia Peter
Afisa Habari (ACT Wazalendo
Leo Oktoba 30,2021.
0 Comments