RPC Iringa Juma Bwire
JESHI la polisi mkoani Iringa limefanikiwa kuwakamata vijana 20 na kuendelea kumsaka kiongozi wa vijana hao wanaofanya kazi ya kuendesha pikipiki (boda boda) maarufu kwa jina la Panya Road ambao wanatuhumiwa kwa makosa mbali mbali yakiwemo ya kiuhalifu na kumfanyia fujo mkaguzi wa jeshi la Polisi Insepekta Said Tolage akiwa kazini .
kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire aliwaeleza waandishi wa habari leo ofisini kwake kuwa jeshi hilo limeendelea na oparesheni mbali mbali kwa lengo la kuzuia na kuondoa uhalifu .
Alisema katika oparesheni iliyofanyika toka Oct 8 mwaka huu majira ya 4 asubuhi hadi saa 11 jioni katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Iringa polisi walifanikiwa kuwakamata vijana hao 20 wanaojiita Panya Road ambao wote wakituhumiwa kwa kosa la kufanya fujo kwa mkaguzi wa polisi na askari wa vyeo mbali mbali .
" Askari hao kwa pamoja walishambuliwa vijana hao wa panya Road wakati vijana hao wakijaribu kuziondosha pikipiki zilizikuwa zimekamatwa kwa makosa ya usalama barabarani siku ya tarehe 8 huko maeneo ya Kisima cha bibi mlima wa Ipogolo askari walikuwa kazini wakitekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria "
Alisema kati ya watuhumiwa wanaosakwa yupo mmoja ambae ni kiongozi wao ambae nyumbani kwake kumekutwa vitu mbali mbali vya kiuhalifu pamoja na bangi za kutosha .
Kamanda Bwire alisema watuhumiwa wote wapo mahabusu na msako mkali unaendelea kufanyika kuwasaka washiriki wengine ambao walifanikiwa kutoweka na pindi watakapo kamatwa watafikishwa mahakamani .





0 Comments