Na, Titus Mwombeki- MDTV BUKOBA.
Mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa iliyopokea chanjo ya UVIKO 19 jumla ya dozi elfu 45 za chanjo aina ya Johnson Johnson kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge amesema kuwa dozi elfu 45 za UVIKO 19 zilizoletwa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo na tayari dozi hizo zimeisha.
“ Kama mnakumbuka kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri jeshi mkuu Samia Suluhu Hassan aliona alete dozi ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 nchini, na sisi katika mkoa wetu wa Kagera tarehe 02/08/2021 tuliletewa dozi elf 45 na zoezi lilizinduliwa rasmi 04/08/2021, kwa furaha kubwa hadi tarehe 10/10/ 2021 dozi hii imemalizika.”
Aidha, amesema kuwa hatua inayofuata ni dozi nyingine ambayo italetwa kwani wananchi wa mkoa huo wameshatambua umuhimu wa dozi hiyo.
“Hatua inayofuata ni dozi nyingine kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huu wa UVIKO 19 kwani wananchi wa mkoa wa Kagera wameishajua umuhimu wa chanjo hiyo”.
Amehitimisha kwa kusema kuwa, wananchi wa mkoa wa Kagera wanatakiwa kuwa makini na watu wasioitakia mema nchi ya Tanzania kwa kueneza habari za upotoshaji kwao juu ya chanjo hiyo.





0 Comments