Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA BUSHIRI ALIA NA WALEMAVU NA WAZEE.

 



NA WILLIUM PAUL, Moshi. 

WANANCHI wameshauriwa kutowaficha watu wenye ulemavu na wazee wakati serikali itakapofanya Sensa ya watu na makazi mwakani kwani nao wanahaki zao za msingi wanazotakiwa kupewa na serikalini. 

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri alipozungumza na wanawake wa kata ya Mji Mpya manispaa ya Moshi ambapo alisema kuwa sensa inaisaidia serikali kutambua inawatu wangapi ili iweze kuwahudumia. 

Zuena alisema kuwa, serikali inania njema hivyo kila mwananchi anawajibu wa kuhesabiwa na kutoa wito wananchi kutowaficha walemavu na wazee.



"Mama unapotaka kupika chakula nyumbani ni lazima ujue kwanza idadi ya watu waliopo ili upike chakula kinachotosha hivyo na serikali inataka kujua idadi ya wananchi wake ili kujua kama huduma inayoitoa na idadi ya watu iliyopo eneo husika je inatosha" alisema Mbunge Zuena.

Akizungumzia swala la chanjo ya UVIKO 19, Mbunge huyo alisema kuwa miongoni mwa mikoa ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni Kilimanjaro ambapo serikali ya awamu ya sita katika kuwajali wananchi wake imeleta chanjo ambayo imethibitishwa na wataalam wa afya kuwa ni salama. 

Alisema kuwa,  kumekuwepo na maneno ya upotoshaji kuwa mtu akichanjwa atageuka kuwa zombo na kusema kuwa maneno hayo ni ya uongozi kwani wananchi wake wakiwamo viongozi wa Kitaifa wameshachanja na mpaka sasa afya zao zinazidi kuimarika.

"Serikali ya mama Samia Suluhu Hasani inawapenda sana haiwezi kuwaletea chanjo zenye madhara na ndio maana kuthibitisha kuwa ni salama alianza kwa kuchanja yeye mwenyewe hivo niwasihi kwa wale ambao hatujachanja tukachanje" alisema Mbunge Zuena. 


Akizungumzia swala la mikopo ya wanawake,  vijana na walemavu ambayo ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya kila halmashauri alisema kuwa,  Rais Samia ameamua kutoa keki hiyo ndogo kila mmoja aweze kuifaida. 

Alisema kuwa,  ipo changamoto ya Vijana kurudi nyuma kwa kutochangamkia fursa hiyo ya mikopo isiyo na riba na kuwataka wakinamama kukaa chini na vijana wao na kuwaelimisha waweze kunufaika na fedha hizo. 

Mwisho... 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI