MSHIKIMSHIKE wa kinyanganyiro cha ligi ya michuano ya Uhalifu Haulipi umefikia patamu huku timu ya Wakulungwa ikiisambaratisha timu ya Bodaboda kwa magoli 2-0.
Wakulungwa wamejihakikishia kuingia hatua ya fainali kutokana na ushindi huo kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Bwawani Kibaha.
Kesho nusu fainali ya pili itapigwa kesho kwenye uwanja huo huo kwa timu za Kiswamba Eletronics na Wagosi ambapo mshindi atachuana na Wakulungwa hatua ya fainali ili kupata bingwa.
Michuano hiyo ambayo imeandaliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani itafikia tamati siku ya Ijumaa kwenye uwanja huo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani wameandaa mashindano hayo ili kuhamasisha wananchi kushirikiana na Jeshi hilo kudhibiti uhalifu.
0 Comments