Mbunge wa Wilaya ya Kilolo Mhe; Justine Nyamoga amewapongeza jumuiya ya wazazi ccm wilaya ya Kilolo kwa jitihada za kuendesha shughuli zao wanazozifanya katika kijiji chao.
Hayo aliyasema alipokuwa mgeni rasmi katika kikao maalumu cha kupokea taarifa mbalimbali za utendaji wa kazi katika baraza hilo la jumuiya ya wazazi chama cha mapinduzi wilaya ya Kilolo.
''ni vizuri kufanya vikao kama hivi, kwahiyo ukiona hivi ujue kuna dalili za uhai najua wengine wanakaa miaka hata mitano kuonana ni kazi kwelikweli, hawakutani kabisa mkiuliza watatoa sababu nyingi sana ambazo nyingine hazina mashiko nyingine zinayo lakini kwa namna yoyote ile uhai wa chama au jumuiya yoyote ni kukutana, kuzungumza, kuweka mikakati na hayo mambo yote mengine sawa'' alisema Mhe Nyamoga.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndugu Yohanes Sarufu alisema kuwa wanampongeza Mbunge wao kwa kipindi kifupi sana cha uongozi wake ameweza kufanya mambo mengi mazuri kwenye jimbo lake, pia amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe; Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake kwa jitihada walizozifanya za kumalizia miradi ambayo iliachwa na Hayati John Pombe Magufuli hususani kwa wilaya ya kilolo, pia ameiomba serikali iwakamilishie barabara ambazo bado hazijakamilika kwani kipindi cha mvua wanapata tabu sana kupita.
''sisi kama jumuiya ya wazazi tuna kila aina ya sababu ya kumshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu kwa jitihada nyingi alizokuwa akizifanya kwa ajili ya kutuletea maendeleo mengi katika wilaya yetu ya kilolo miradi ya elimu, afya, maji, barabara kwa sababu ni wilaya ambayo ipo pembezoni sana mwa mkoa huu na ina miundombinu ambayo ni migumu hasa ukilinganisha kuna milima na kuna mvua nyingi kiasi ambacho kipindi cha masika njia nyingi hazipitiki pamoja na jitihada za kuleta barabara za rami,'' alisema Sarufu
Na kwa upande wake, Katibu wa Jumuiya Ndugu Ahmed Gimbo, akisoma taarifa fupi amesema kuwa wilaya ya kilolo ina matawi 157 ya Chama Cha Mapinduzi, kata 25 za kichama, huku serikali ikiwa na kata 24 na tarafa 3 ambazo ni Kilolo, Mazombe na Mahenge, huku kata ya kilolo ikiwa na jimbo moja la uchaguzi ambalo linashikiliwa na chama cha mapinduzi.
0 Comments