Header Ads Widget

JKT 821 BULOMBORA KULIMA HEKALI 2000 ZA MICHIKI



Na Mwandishi wetu, Kigoma


Kikosi cha Jeshi 821 JKT Bulombora kimepanda miche ya michikichi zaidi ya hekali 500 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Akizungumza na wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Tari Kamanda wa kikosi cha jeshi 821 Bulombora Luten Kanal Emanuel Kakula alisema kuwa wamepewa jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa wanapanda hekali 2000 hali ambayo imeanza kutekelezwa kwa kupanda 500.


“Tulipewa jukumu la kupanda michikichi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa tumepokea vizuri ikiwa ni muhimu kwa uzalishaji wa michikichi ambapo wananufaika kwa kupanda michikichi ambapo wanafundishwa namna gani wanahudumia michikichi kuanzia mbegu hadi unapoenda shambani”


“Sisi tunazalisha miche tunagaia wananchi lakini pia tunapanda wenyewe hili ni zao muhimu kwa nchi yetu hata ukiangalia tunaovijana kutoka mikoa mbalimbali wanapata mafunzo hapa wanapata mafunzo ya awali ya kijeshi na stadi za maisha”


Msaidizi wa bwana shamba 821KJT Bulombora Ombeni Mushi alisema kuwa wamejipanga kupanda miche ya michikichi aina ya tenera kwa awamu ambapo awamu ya kwanza tayari heka 500 zimepandwa.


“Watafiti wa Tari Kihinga mwaka jana walitupatia mbegu laki mbili na sisi tulipewa lengo la kuotesha mbegu hekali 2000 tumeanza kutekeleza kwakupanda miche 500 iliyobakia tutazikamilisha kwa awamu hata hivyo tumetoa miche kwa wananchi bure”


 “Sisi tunayofaida kubwa tunaovijana wanapata mafunzo hapa wanapata faida kubwa sana wapo walioanzisha mashamba na kuja kuchukua mbegu hapa lakini” alisema Luten kanal Kakulu


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI