WAKATI JATU PLC ikiadhimisha miaka 5 tangu kuazishwa kwake Serikali imesema kunahaja ya kupitia Sera na Sheria zinazo wahusu vijana na kuangali upya mipango yote iliyopo ndani ya serikali ili kuona kama zinawawezeshe na kuwapa dira vijana wa kitanzania kusongambele. Mwandishi Hamida Ramadhan Dodoma
Akizungumza jijini Dodoma katika sherehe za Miaka 5 ya Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (JATU PLC) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshugulikia Sera, Bunge,kazi,Ajira, vijana na watu wenye walemavu Jenista Mhagama amesema ipo haja kubwa ya kupitia sheria zote zinazowahusu vijana kama zinatengeneza fursa nzuri za kuwawezesha vijana kuweza kuendelea na kusonga mbele.
Pia amesema anakwenda kuangalia mipango yote iliyomo ndani ya serikali kama zimeweka mipango mizuri za kuwezesha vijana wachakalikaji kufikia malengo ya kuhakikusha taifa taifa linaondokana na umasikini kama mipango yetu ndani ya nchi.
Amesema kwa mara ya kawanza alikutana na vijana watatu Simiyu katika Wiki ya vijana nasasa JATU wamekuwa wakikua kama mti mkubwa utakao weza kuliwa matunda na watanzania wote.
"Ni ukweli usiopingika watanzania wakiamua wanaweza na kupitia vijana wa JATU PLC hakika wamefungua njia na kuonyesha kuwa ndani ya taifa letu tunamtaji mkubwa watakao weza kuleta Maendeleo ndani ya taifa hili na mimi.nitakuwa na nyiyi vijana wa JATU bega kwa bega," amesema Mhagama.
Aidha ametoa wito kwa vijana hao wa JATU PLC kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani kumekuwa na kasumba ya vijana wengi wakushajulikana na kupata mafanikio kidogo .
" Msipokuwa na Nidhamu mtaanfuka na anguko lenu litakuwa kubwa kuliko hapa mlipofikia ni muombe Mwenyekiti wa Bodi awasaidie sana kwani nyiyi vijana wa JATU ni mfano mzuri katika jamii," amesema Waziri Muhagama.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni maalumu katika sherehe hiyo amewataka vijana wa JATU PLC kusonga mbele na kuachana na habari ya vijiweni kuwa kilimo au ufugaji haulipi.
" Huu ni mwanzo mzuri kwa vijana wetu wa kitanzania japo kilimo kimekuwa cha kukatisha tamaa lakini nyiyi vijana wa JATU PLC mlisonga mbele na leo tunaona matunda yenu kutoka mtaji wa Bilioni 1 hadi leo mtaji wa Bilioni 14 Hongereni sana," Amesema Waziri Mstaafu Pinda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu JATU Mohamed Simbano amesema Malengo ya JATU ni kuhakikisha wanainua maisha ya kila Mtanzania lishe na usalama wa chakula ambapo kampuni hiyo imeshatoa ajira za kudumu kwa jina 500 na ajira zaidi ya Elfu 10 zisizo za kudumu wa watanzania.
Pia amesema JATU ni kimbilio la wengi kwani kwasasa kampuni hiyo imejikita katika kilimo na ufugaji ambapo kuanzia mwaka 2022 hadi mwaka 2023 wataanza kulima mazao ya aina tatu ambayo ni Maharage, Mahindi na Alizeti lakini pia katika kukabiliana na mabadiliki ya tabia ya nchinwameanza kilimo cha umwagiliaji Kiteto.
Naye Peter Gasaya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU amesema Dira yao kwa miaka 10 ijayo ni pamoja na Kuanzisha Benki kubwa ya kibiashara huku Katibu Mkuu wa Kampuni hiyo
Amesema kama jamii ingekuwa na uelewa wakutosha wangekuwa na miradi mingi hiyo ni kutokana na mifumo ya sheria katika ngazi za Serikali za mitaa hasa ngazi za Kata kumekuwa na migongano kuhusu masuala ya kisheria na hivyo kukinzana na kufanya wao kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Hata hivyo kampuni ya JATU inajihusisha na kilimo Jumuishi pamoja na kutafuta maeneo mazuri ya uwekezaji ambapo Mwaka 2016hadi2021 imewekeza ekari 5000kwa Vijana kwaajili ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo ya kilimo lengo ni kuwafikia watu milioni2 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.





0 Comments