Header Ads Widget

DC ABDALLAH MWAIPAYA ATAKA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA WATOTO


 WAZAZI wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusimamia maadili ya watoto wao badala ya kuwaachia walimu peke yao.


Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdala Mwaipaya wakati wa mahafali ya kidato cha nne kwenye shule ya Vuchama Ugweno Islamic.


Mwaipaya alisema kuwa ili wanafunzi waweze kufanya vyema kwenye masomo yao lazima kuwe ushirikiano baina ya wazazi na walimu.


Alisema kuwa wazazi nao wanasehemu ya ufaulu wa wanafunzi hivyo nao wanapaswa kushiriki kwa kuwafuatilia masomo yao na si kuwaachia walimu peke yake.


Aidha amewataka wanafunzi hao wanaomaliza elimu ya Sekondari wazingatie maadili mema wanayofundishwa shuleni ili kuwa na Taifa na viongozi bora.



"Maadili mliyoyapata muende nayo msije mkabadilika na kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa na kusababisha kufanya vibaya kwenye masomo na kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya mwisho,"alisema Mwaipaja.


Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanalipa ada kwa wakati ili shule hizo ziweze kujiendesha kwani zinategemea ada kama sehemu ya kujiendesha na hazina ruzuku.



Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Jumanne Mkoga alisema kuwa changamoto kubwa shuleni hapo ni kukosa uzio hali ambayo inasababisha kuwe na muingiliano na watu wasio wanafunzi.


Mkoga alisema kuwa muingiliano huo husababisha wizi na kuingiza kwa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na dawa za kulevya kama bangi na kufanya vitendo vibaya.


Awali meneja wa shule hiyo Yasin Mfinanga alisema wanaomba ushirikiano na serikali ili kuwapatia wanafunzi kwani wao wana madarasa ya kutosha tofauti na shule za serikali ambazo zinaupungufu wa vyumba vya madarasa.

Mfinanga alisema kuwa ili kuboresha sekta ya elimu ni vema kukawa na ushirikiano baina serikali na sekta binafsi kwa kuwapunguzia wanafunzi wanaokosa nafasi.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI