Header Ads Widget

🛑BREAKING:MOTO WATEKETEZA BWENI KITUO CHA YATIMA HURUMA KINACHOMILIKIWA NA KKKT IRINGA

 MOTO mkubwa ambao chanzo chake hakikafahamika umeteteteza bweni la vyumba vinne Katika Kituo cha kulea watoto Yatima cha Huruma Center kinachomilikiwa na kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)dayosisi ya Iringa.


Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na matukio Daima Blog walisema  kuwa moto huo ulianza kuwaka Majira ya saa 9 Alasiri ya  leo  na kuwa hawajui chanzo chake .

Amina Sanga mkazi wa eneo  Hilo alisema wakati moto huo unaanza kuwaka alikuwa akipita jirani na kituo hicho na alijua Kuna takataka zinachomwa jirani na kituo .

"Sikujua kama ni bweni linawaka moto ila baada ya kusogea ndipo nilibaini kuwa ni Moto unawaka "

Huku afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Tina Mbaga alisema kuwa bweni hilo lililuwa linatumiwa na watoto 11 ila wakati moto unawaka ni watoto 6 pekee ndio walikuwa wamerejea shule na wote wapo salama .


Diwani wa kata ya Mwangata Galusi Lugenge alisema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na jeshi la zimamoto na uokoaji Iringa kuthibiti moto huo .

Pia aliwashukuru wananchi ambao walianza kuzima moto huo Kwa Maji Kwa kutumia ndoo za Maji .

Mkuu wa kituo hicho mchungaji Joyce Ngandango alisema kuwa Hadi Sasa hasara ya moto huo ni kubwa na kuwa mali nyingi zimeteketea Kwa moto pamoja Chumba cha stoo .

Mchungaji huyo alisema moto ulianza kuwaka juu ya paa na ulianza Chumba cha watoto wadogo kabisa na ndio waliopiga kelele kuwa moto unawaka japo watoto wote wapo salama .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire hakuweza kupatikana kuelezea undani wa tukio hilo.

Habari zaidi tembelea Chaneli ya Matukio Daima Tv tupo Live eneo la tukio

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI