Picha ya maktaba
Mwananchi anayefahamika kwa jina moja la Bahati Mkazi wa Kijiji cha Ukondamoyo Wilaya ya Urambo mkoani Tabora ameuawa na Watu wanasiojulikana kwa kushambuliwa na mapanga kutokana na kushindwa kuwapa milioni tano walizozitaka baada ya kumvamia nyumbani kwake.
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Rahabona Bitashika amesema Watu hao waliingia nyumbani kwa Bahati usiku wa saa 8 kisha kumwamuru atoe shilingi milioni 5 na aliposhindwa kuwapa wakamuua ambapo Bahati alifariki akiwa njiani kuwaishwa Hospitalini.
Imeelezwa kwamba Marehemu Bahati ameacha Wake kumi na wa tatu (13) ambapo wanane katika yao wanaishi kwenye kaya moja na wengine watano wanaishi sehemu nyingine
0 Comments