Header Ads Widget

Alec Baldwin: Bunduki zinazotumiwa katika uigizaji ni zipi na je ni hatari?


A gun is loaded with ammunition

Polisi inasema muigizaji filamu wa Marekani Alec Baldwin alifyatua risasi iliyomuua mwandishi wa sinema Halyna Hutchins na kumjeruhi mwelekezaji Joel Souza kwenye maandalizi ya filamu mjini New Mexico. Walikuwa wakifanyia kazi filamu ya Rust.

Heshima zimetolewa kwa Bi Hutchins, 42, wakati Bw Baldwin anasemekana kufadhaika. Gazeti moja limeripoti kumpata akilia machozi nje ya Ofisi ya polisi ya Kaunti ya Santa Fe.

Uchunguzi unaendelea na hatujui ni nini kilichotokea. Msemaji wa Bw. Baldwin amesema ajali imetokea kwenye seti inayohusisha upigaji risasi wa bunduki na risasi ya uigizaji.

Ijapokua silaha hizo sio halisi zinaweza kuwa hatari. Haya ndio baadhi ya mambo tunayojua kuzihusu.

Bunduki za uigizaji ni zipi?

Bunduki bandia hutumiwa katika filamu kuigiza bunduki halisi.

Kile ambacho hufanya bunduki hizo kuonekana kama bunduki halisi ni kuwa zimeundwa kutokana na risasi halisi.

Risasi za kisasa zinatengenezwa na cartridge, ambayo ina sehemu ya kushikilia maganda ya risasi.

Wakati bunduki inapopiga risasi, inawasha moto, na kurusha risasi iliyowekwa mbele ya ganda.

A graphic showing how blank cartridges work

Badala ya kutumia makadirio ya chuma, nafasi zilizo wazi zina nyenzo kama pamba au karatasi iliyowekwa mbele.

Silaha hizo kwa Pamoja zinaongeza uhalisia katika filamu - ukifyatua risasi kwa kutumia bunduki ya uigizaji, utasikia mlio mkubwa na kurudishwa nyuma

Je tukio kama hili lishwahi kutokea?

Ndio. Huenda unamkumbuka Brandon Lee, mwana wa kiume wa muigizaji mkongwe wa filamu za vita Bruce Lee.

Brandon Lee alifariki akiwa na miaka 28 mnamo 1993 akirekodi filamu ya The Crow, baada ya bunduki inayotumiwa katika uigizaji iliyokuwa na risasi kimakosa kuelekezwa kwake.

Risasi bandia hazina vilipuzi na wakati huo ilikuwa inatumika kunasa tukio la filamu kwa karibu zaidi. Wakati risasi za uigizaji zilipokuwa zinawekwa katika bunduki risasi halisi zilisahaulika ndani ya bunduki kwa bahati mbaya.

Baada ya Lee kupigwa risasi, kamera iliendelea kurekodi tukio. Ilijulikana kuna kitu kimetokea mwisho wa kurekodi kwani muigizaji hakuamka.

Katika tukio jingine mwaka 1984, muigizaji wa Marekani Jon-Erik Hexum alianza kufanya mzaha kwenye seti ya kipindi cha televisheni baada ya kuchoka kusubiri muda wa kurekodi filamu.

Aliweka risasi bandia katika bunduki aina ya revolver, na kujielekezea kichwani na kufyatua risasi.

Tofauti na Lee, hakuuawa na projectile, lakini nguvu ya mlipuko ulikuwa mzito kiasa cha kuvunja fuvu lake la kichwa. Alifariki baadaye akiwa hospitali.

Bunduki zisizokuwa na risasi na vifaa vingine vinawezaje kutumiwa kwa usalama

Kifo cha Hexum kinaangazia matatizo ya bunduki bila risasi- hata bila ya kuwa na ncha ya risassi huwa zinawekwa poda nyingi .

Kitu cha hatari zaidi ni kwamba baadhi ya seti za filamu zinatumia poda ya ziada ya risasi ili kuongezea uhalisia wa mlipuko kwenye filamu.

Seti za filamu huwa na masharti makali kuhusu namna ya kutumia bunduki ya kuigiza. Wataalamu huleta silaha zitakazotumiwa na kutoa ushauri wa jinsi ya kuzitumia.

Kuna hatua za msingi za usalama kwenye kila seti," alisema Tristano, mtunza silaha ambaye aliwahi kufanya kazi na Alec Baldwin zamani.

"Usielekeze bunduki kwa mtu hata kama haupigi risasi. Sielewi jinsi ajali hii lilitokea na kusababisha maafa."

Wengine walihoji kwanini, wakati huu ambao mlio wa bunduki unaweza kujumuishwa kwenye filamu kwa kutumia kompyuta , bado bunduki ya kuigiza zinatumika.

"Hakuna sababu ya bunduki iliyojazwa risasi bandia au kitu kingine kutumika kwenye seti ya filamu. Hii inafaa kuharamishwa kabisa,"aliandika kwenye ujumbe wa Twiter Craig Zobel, muigizaji na mwelekezaji wa filamu ambaye amewahi kushiriki katika filamu ya Westworld na Mare of Easttown.

''Bunduki ya uigizaji ni bunduki halisi, mwandishi wa televisheni David Slack aliandika. "risasi bandia zinanatumia poda halisi ya risasi. Zinaweza kuumiza au kuaa- na zishawahi kufanya hivyo. Ukiwahi kuuwa kwenye seti ya filamu ambapo bunduki ya kuigiza inatumika bila kuzingatia usalama unaostahili, achana na hiyo kazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI