Moyo amesema hayo usiku huu alipozungumza na Matukio Daima media kwa njia ya simu ,alisema tayari ofisi yake na jeshi la polisi wanafuatilia undani wa taarifa hizo kwa kwenda eneo la tukio .
Huu ni ujumbe unaosambaa kwa kasi kwenye makundi ya WhatsApp usiku huu .
"Habarini za wakati huu...Jamani kama mna ndugu,jamaa na Marafiki waliokuwa wanasafiri leo na Basi la Kampuni ya ISAMILO linalofanya safari zake toka Mwanza kuelekea Mbeya.Basi hilo la ISAMILO limepata ajalj hapa maeneo ya kijiji cha Izazi mkoani Iringa majira ya usiku huu.....Fanyeni Mawasiliano na wapendwa wenu ili kujua hali zao maana kuna waliojeruhiwa na kupoteza maisha pia ktk ajali hiyo.... *TUSAMBAZE TAARIFA HII KTK GROUP ZETU ZOTE*🙏🏽🙏🏽"
Matukio Daima tunaendelea kufuatilia undani wa taarifa hizi kupitia jeshi la polisi na ofisi zenye mamlaka ya kutoa taarifa ili kujua undani wake .
Endelea kuwa nasi .
0 Comments