Wasafiri wanaokwenda jijini Dar es Salaam na kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini kama Iringa ,Mbeya ,Njombe ,Songwe,Rukwa na nchi za Malawi ,Afrika kusini na Zambia na Ruvuma wamekwama Kwa muda eneo la Mlima Kitonga wilaya ya Kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa -Morogoro baada ya Malori mawili kuziba barabara Kwa ubovu .
Tukio Hilo limetokea toka alfajiri ya Leo Hali iliyopelekea mabasi ya abiria kukwama Kwa muda eneo hilo Hadi saa 2.30 barabara hiyo ilipofunguliwa .
Wakizungumza na matukio Daima madereva eneo hilo wamedai chanzo ni Malori mawili kutaka Kulazimisha kuyapita Malori mengine ya mbele Hali iliyopelekea Malori hayo kukwama mlimani na kuziba njia .
Kutokana na kadhia hiyo wasafiri wameomba jeshi la polisi Kikosi cha usalama barabarani Iringa kuweka ulinzi mkali kwenye Mlima huo ili Malori kufuata Sheria za usalama barabarani kwani ni hatari Kwa wasafiri Kwa madereva hao kuvunja sheria eneo hilo.
0 Comments