Matokeo ya shambulio la ndege isiyo na rubani katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul
Serikali ya Marekani imejitolea kuwafidia jamaa za wahasiriwa waliouawa kimakosa katika shambulio la ndege isiyo ya rubani iliyofanywa na majeshi yake dhidi ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, mwezi Augosti.
Mfanyakazi wa kutoa msaada na jamaa tisa wa familia yake, wakiwemo watoto saba, walifariki katika shambulio hilo.
Pentagon ilisema inafanya kazi kusaidia jamaa wa familia hiyo walionusurika kuhamia Marekani.
Shambulio hilo lilifanyika kabla ya Marekani kuondoa vikosi vyake nchini humo.
Ilikuja wakati wa juhudi kubwa ya kuwaokoa watu kufuatia kurudi kwa ghafla kwa Taliban na siku chache tu baada ya shambulio baya karibu na uwanja wa ndege wa Kabul lililofanywa na IS-K, tawi la kundi la Islamic State (IS).
Majasusi wa Mareakani walikua wamefuatilia gari la mfanyakazi huyo wakutoa msaada kwa saa nane mnamo Agosti 29, ikiamini kwamba alikuwana uhusiano nawanamgambo wa IS-K, alisema mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerali Kenneth McKenzie mwezi uliyopita.
Uchunguzi ulibaini kuwa gari hilo lilikua limeonekana katika makazi yanayohusishwa na IS-K, na harakati zake ziliwiana na ujasusi mwingine kuhusu mipango ya kundi yala kigaidi ya shambulia uwanja wa ndege wa Kabul.
Wakati mmoja, kifaa cha ufuatiliaji kiliona wanaume wakipakia kile kilichoonekana kuwa vilipuzi kwenye buti ya gari, lakini zikagunduliwakuwa kawa vyombo vya kuteka maji.
Jenerali McKenzie alielezea shambulio hilo kuwa "makosa mabaya" na kuongeza kuwa Taliban hawakuhusika katika ujasusi uliosababisha shambulio hilo.
Shambulio lilitokea wakati mfanyakazi wakutoa msaada - kwa jina Zamairi Ahmadi -alipoegesha gari nyumbani kwake , kilo mita tatu kutoka uwanja wandege wa Kabul.
Mlipuko huo ulianzisha mlipuko wa pili, ambao maafisa wa Marekani hapo awali walisema ni ushahidi kwamba kweli gari hilo lilikuwa limebeba vilipuzi. Hata hivyo, uchunguzi umebaini kuwa huenda ulisababishwa na mtungi wa gesi iliyokuwa kwenye barabara ya gari.
Mmoja wa waliouawa ni, Ahmad Naser, ambaye alikuwa mkalimani wa vikosi vya Marekani. Wengine ni waliwahi kufanyia kazi mashirika ya kimataifa na walikuwa na visa ya kuwaruhusu kuingia Marekani.
Tangazo la kuwalipa fidia watu hao lilitolewa Alhamisi wakati wa mkutano kati ya Colin Kahl, katibu ulinzi wa sera, na and Steven Kwon,mwanzilishi na rais wa kundi la msaada la Nutrition and Education International ambalo lilikua likiendesha shughuli zake nchini Afghanistan, Pentagon ilisema katika taarifa.
Bw. Kahl alisema kwamba bwana Ahmadi na wenzake waliouawa "hawakua na hatia na kwamba hawakua na uhusiano wowote na wanamgambo wa ISIS-K au tisho kwa vikosi vya Marekani", alisema taarifa hiyo kutoka kwa msemaji wa wizara ya ulizni said a John Kirby.
0 Comments