Header Ads Widget

SWALA WA TANAPA AMPIGA MWEREKA TEMBO WA TAWA KWENYE MASHINDANO YA SHIMMUTA 2025 MOROGORO


Timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imeingia hatua ya robo fainali leo tarehe 2/12/2025 baada ya kupata ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya wapinzani wao Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) katika mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea Mkoani Morogoro.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa umeonyesha ubora na umakini wa kikosi cha TANAPA, ambacho kiliweza kudhibiti mchezo na kutumia vizuri nafasi muhimu zilizozaa ushindi.

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu TANAPA, Ramadhan Okello, amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma, kupambania nembo ya shirika na kufuata maelekezo kwa nidhamu uwanjani. Ameeleza kuwa ushindi huu ni matokeo ya maandalizi mazuri, umoja wa timu na morali ya juu ndani ya kikosi.

Timu ya TANAPA sasa inaelekeza nguvu katika mchezo ujao wa robo fainali dhidi ya Shirika la Mzinga, huku ikiwa na dhamira moja—kuendelea kuonyesha ubora, kupigania heshima ya shirika na kufikia hatua ya nusu fainali.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI