Header Ads Widget

OFISI YA WAZIRI MKUU-TAMISEMI KUSHUGHULIKIA WATUMISHI WAZEMBE




Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Mhe. Reuben Kwagilwa, amesisitiza kuwa ofisi hiyo itaendelea kuchukua hatua kwa watumishi wazembe na wanaotumia vibaya fedha za Serikali. 

Akizungumza wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba mkoani Songwe, Mhe. Kwagilwa ameeleza kwamba ofisi hiyo itafika katika Halmashauri zote nchini ili kuhakikisha watumishi wanaofuja fedha za Serikali katika miradi ya maendeleo wanawajibishwa ipasavyo. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI inasisitiza dhamira yake ya kuhakikisha kwamba fedha za Serikali zinatumiwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya maendeleo ya jamii,” aliongeza Mhe. Kwagilwa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI