Header Ads Widget

ZELENSKY:PUTIN ALIPATA KILE ALICHOTAKA KATIKA MKUTANO WA ALASKA NA TRUMP

 


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameliamba shirika la habari la ABC kwamba mkutano wa Rais Donald Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin uliofanyika Alaska ulimpa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin kile alichotaka.

"Ni aibu kwamba Ukraine haikuwepo kwasababu nadhani Rais Trump alimpa Putin kile alichotaka," Zelensky alisema. "Alitaka sana kukutana na Rais Trump, na rais wa Marekani. Na nadhani Putin alifikia hilo . Na hiyo ni aibu."

Zelensky alifanya mahojiano na mwandishi mkuu wa masuala ya kimataifa wa ABC News Martha Raddatz siku ya Ijumaa, ambayo yalitangazwa i kwenye kipindi cha ABC News "Wiki hii."

"Putin hataki kukutana nami, lakini anataka kukutana na rais wa Marekani ili kuonyesha kila mtu video na picha za uwepo wake," rais wa Ukraine alisema.

Akizungumzia uwezekano wa kukutana na Putin, Zelensky alisema kuwa rais wa Urusi alikuwa ametoa masharti ya mkutano huo ambayo hangeweza kuyakubali na kwamba Putin "alikuwa akicheza michezo na Marekani."

"Alisema alisema atakutana nawe kama utakuja Moscow," Raddatz alimwambia Zelensky.

Zelensky alicheka. "Anaweza kuja Kyiv," alisema, na kuongeza: "Siwezi kwenda Moscow wakati nchi yangu inapigwa na roketi na mashambulizi kila siku."

Raddatz alipouliza ni nini angechukulia kuwa ushindi kwa nchi yake, Zelensky alijibu kwamba ni kuishi kwa Ukraine.

"Lengo la Putin ni kuikalia Ukraine," Zelensky alisema. "[Putin] hakika anataka kutuchukua kabisa. Kwake, huo ni ushindi. Na hadi afanye hivyo, ushindi uko upande wetu. Kwa hivyo kwetu, kuishi ni ushindi. Kwasababu tunaishi kwa kuhifadhi utambulisho wetu, nchi yetu, uhuru wetu."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI