Header Ads Widget

WAFUNGWA WA KIPALESTINA HAWAPEWI CHAKULA CHA KUTOSHA-MAHAKAMA YA ISRAEL

 

Mahakama ya Juu ya Israel imetoa hitimisho kuwa taifa hilo linashindwa kuwapa chakula cha kutosha wafungwa wa Kipalestina, na lazima lichukue hatua za kuboresha lishe yao.

Majaji watatu walisema siku ya Jumapili kwamba serikali ya Israel ina wajibu wa kisheria kuwapa wafungwa chakula cha kutosha.

Maelfu ya Wapalestina wamezuiliwa katika jela za Israel kwa miaka mingi, ikiwa ni pamoja na mashtaka ya ugaidi - na maelfu ya wengine wamezuiliwa tangu vita vya Gaza kuanza Oktoba 2023.

Mazungumzo ya kusitisha mapigano yamekwama lakini Jumapili usiku Rais wa Marekani Donald Trump alitoa "onyo la mwisho" kwa Hamas, akiwataka kukubali makubaliano ya kuwaachilia mateka wa Israel kutoka Gaza.

Hamas ilijibu katika taarifa na kusema iko tayari "kuketi mara moja kwenye meza ya mazungumzo" kufuatia "mawazo kutoka upande wa Marekani yenye lengo la kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano".

Wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa huru wameiambia BBC walitendewa vibaya na kuteswa mikononi mwa wanajeshi wa Israel na wafanyakazi wa magereza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI