Header Ads Widget

MWANAMKE ALIYEWAUA WAKWE ZAKE AFUNGWA MIAKA 33

 

Mwanamke raia wa Australia aliyepatikana na hatia ya kuwaua jamaa watatu wa mume wake walioachana kwa kuwapa chakula chenye uyoga wenye sumu amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela siku ya Jumatatu, katika mojawapo ya vifungo virefu zaidi kuwahi kutolewa kwa mwanamke nchini humo.

Hakimu mfawidhi alisema Erin Patterson (50) hakuwahurumia wakwe zake wazee baada ya kuwapa nyama ya Ng'ombe iliyotiwa uyoga wenye sumu.

Patterson alipatikana na hatia mwezi Julai kwa kumuua mama mkwe wake, Gail Patterson, baba mkwe, Donald Patterson na dadake Gail, Heather Wilkinson, katika kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa duniani kote na kupewa jina la mauaji ya uyoga.

Baraza la majaji pia lilimpata na hatia ya jaribio la kumuua Ian Wilkinson, mume wa Heather, ambaye alinusurika mwaka 2023 nyumbani kwa Patterson huko Leongatha, mji wa ulio kilomita 135 (maili 84) kusini mashariki mwa Melbourne.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI