Header Ads Widget

JESHI LA ISRAEL LAWAAMURU 'WAKAZI WOTE' WA GAZA CITY KUHAMA MARA MOJA

 

Jeshi la Israel linawaamuru "wakaazi wote" wa mji wa Gaza kuhama kabla ya mashambulizi mapya, baada ya Israel kuonya kuwa itaongeza mashambulizi yake ya kijeshi katika ukanda huo ikiwa Hamas haitawaachilia mateka wa mwisho inaowashikilia.

Katika chapisho kwenye X, msemaji wa IDF wa lugha ya Kiarabu anasema kwamba itachukua hatua kwa "nguvu kubwa" katika Jiji la Gaza na kuwaonya wakaazi kuondoka.

"Vikosi vya ulinzi vimedhamiria kuishinda Hamas na vitatenda kwa nguvu kubwa katika eneo la mji wa Gaza," Avichay Adraee amendika.

Haya yanajiri baada ya baraza la mawaziri la usalama la Israel mwezi uliopita kuidhinisha mpango wa kuchukua udhibiti wa mji huo, ambapo mamia ya maelfu ya Wapalestina wanaishi.

Ajith Sunghay, kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu (OHCHR), anaonya operesheni ya Israeli katika mji wa Gaza itakuwa "janga".

"Tunachoenda kuona ni kitu ambacho hatujaona hapo awali ... wanaharibu kila kitu kinachohitajika kwa maisha ya raia," alikiambia kipindi cha BBC, BBC.Newsday

"Miundo yote ya kiraia, iwe ni matanki ya maji, barabara, majengo, yote vimeharibiwa...tumeona katika sehemu ya kaskazini ya Gaza wameisawazisha, na tunahofia kuwa Jiji la Gaza litakabiliwa na matokeo sawa."

Maelfu ya watu watakuwa wakijaribu kuhamia kusini, anasema, lakini asilimia fulani hawatahama.

Wanajua wakiondoka hawataweza kurudi, ameongeza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI