Na Shemsa Mussa -Matukio Daima
KAGERA.
Mgombea mwenza kwa nafasi ya urais Dk Emmanuel Nchimbi amesema katika siku 100 baada ya kumpata Rais Serikali itatoa ajira 5000 za afya,elimu 7000 ili kuendeleza huduma za jamii.
Akizungumza leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashai iliyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ikiwa ni siku ya pili akiwa mkoani humo Kwa ajira kuomba kura kwa wananchi.
Dkt Nchimbi,Amesema Ajira hizo ni kutokana na kuongeza miundombinu ya afya na elimu ndani ya siku 100 mara baada ya kumpata Rais wa jamhuli ya muungano Wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).
Aidha amesema Mgombea nafasi ya urais Dk Samia Suluhu Hassan amekusudia kuanza na tatizo la suala la Bima za afya kwa kuanza na wanawake wajawazito, wazee, watoto na watu wenye ulemavu kwani limekuwa ni tatizo kwa makundi hayo,pia watawasaidia wananchi wenye magonjwa yasiyoambukiza kupata huduma bure za matibabu.
Ameongeza kuwa mipango ijayo ni kuongeza vituo vya afya vipya vya kisasa vitatu vitajengwa Manispaa ya bukoba ikiwamo zahanati nne , shule mpya za msingi madarasa136 pamoja na Miradi ya huduma za umeme kuongezaka.
Katika upande wa miundombinu ya barabara kutakuwa na ujenzi wa jengo la abiria ikiwamo vibanda vipya ikiwa hatua za awali tayari zimeshaanza kufanyiwa ikiwemo stendi.
Amesema kuwa kwenye vikundi vya maendeleo itatengwa sh.bilioni 200kwa ajili ya kukopesha vijana.
Hata hivyo amesema,katika suala la kilimo baada ya uchaguzi Serikali itajenga kiwanda kwa ajili ya kitengemeza mvinyo wa ndizi kitakachowawezesha wakulima Wa ndizi kuepuka hasara pindi ndizi zinapoiva(mbivu) kuharibika.
0 Comments