Header Ads Widget

MAUAJI YA WATU WAWILI MWANZA YATIKISA, POLISI WAANZA UCHUNGUZI.


Na chausiku said Matukio Daima Mwanza.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza kufanya uchunguzi wa matukio mawili ya mauaji yaliyotokea kwa nyakati tofauti, likiwemo tukio la wananchi wenye hasira kali kumshambulia mtuhumiwa hadi kufariki dunia.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,  Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio la kwanza lilitokea baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa na kumshambulia kwa mawe na silaha za jadi. Polisi walifika eneo la tukio na kumnusuru, kisha kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Sekou-Toure kwa matibabu zaidi, lakini alifariki dunia wakati akiendelea kutibiwa.

Amesema miili ya marehemu wote watatu imehifadhiwa hospitalini kwa uchunguzi wa kitaalam, na uchunguzi wa tukio unaendelea. Aidha, amesema wanamshikilia Ustadhi Juma Idd, mganga wa tiba asilia, kwa mahojiano, huku akiwataka waganga wa tiba asilia kutambua historia za wagonjwa wao, kuwashauri na kuwaelekeza wagonjwa wenye maradhi makubwa kwenda hospitali kupata tiba za kitaalam.

Mutafungwa amesema katika tukio jingine lililotokea Agosti 9, 2025 majira ya saa 2:50 asubuhi, mwili wa kijana wa kiume ambaye jina lake halijatambulika , anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30, ulipatikana kando ya barabara ya Luchelele, mtaa wa Malimbe, wilayani Nyamagana, ukiwa na majeraha mikononi na shingoni.

Ameongeza kuwa uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea, na ametoa wito kwa yeyote mwenye taarifa kuwasilisha kwa polisi, viongozi wa serikali au vyombo vingine vya usalama. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa uchunguzi zaidi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI