NA MATUKIO DAIMA MEDIA IRINGA
Matokeo ya kura za maoni kwa watia nia wanaowania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi CCM kugombea ubunge mkoani Iringa wabunge wa majimbo matatu wanaomaliza muda wao na kutetea nafasi zao wamezidiwa kura na watia nia wapya
Matokeo ya uchaguzi katika majimbo ya mkoa huo yamekuwa ni ya furaha kwa watia nia watatu wapya huku yakiwa mwiba mchungu kwa wabunge wanaomaliza muda wao watatu kati yao wakiwemo manaibu Waziri wawili.
jimbo la Isimani aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo William Vangimembe Lukuvi ameongoza kwa kupata kura 5797 Festo Shemu Kiswaga akiwa wapili kwa kupata kura 1159 nafasi ya tatu akiwa ni Sebastian Antony Kiyoyo aliyepata kura 40 nafasi ya nne akiwa Elias Lupito Migodela ambaye pia alipata kura 40 watano ni David Evans Komba aliyepata kura 39 huku Abdallah Suleiman LUSASI akiambulia kura 24 na kushika nafasi ya sita ambapo idadi ya kura zilizopigwa zikiwa 7,223 kura zilizoharibika ni 124 idadi ya kura halali zilikuwa ni 7,099.
Jimbo la Kalenga Idadi ya kura zilizopigwa ni 8,115 idadi ya kura zilizoharibika 103 na idadi ya kura halali zilikuwa 8,012 ambapo katika matokeo aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Jackson Gidion kiswaga alitangazwa kuongoza kwa kupata kura 4036 akifuatiwa na Grace Victor Tendega aliyepata kura 2391 nafasi ya tatu akiwa ni Mussa Leonard Mdede aliyepata kura 1281 na nafasi ya nne ikishikwa na Henry Thomas Nyaulingo aliyepata kura 304
Kwa jimbo la Iringa mjini idadi ya kura zilizopigwa zilikuwa 4,656, Idadi ya kura zilizoharibika zilikuwa 32 na idadi ya kura halali 4,624 huku Fadhili Fadhili Fabian Ngajilo akitangazwa kuongoza kwa kupata kura 1899 wakili Moses Gwatengile Ambindwile akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1523 nafasi ya tatu akishika mchungaji Peter Simon Msigwa kwa kuwa na kura 477 nafasi ya nne akiwa ni mbunge aliyekuwa akitetea nafasi yake Jesca Jonathan Msambatavangu aliyepata kura 408 Nguvu Edward Chengula akishika nafasi ya tano kwa kupata kura 181 huku Islam Nihed Huwel akishika nafasi ya sita kwa kuwa na kura 136.
Jimbo la Kilolo aliyekuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Enespher Kabati ameongoza kwa kupata kura 4565, Novat Atilio Mfalamagoha akiwa wapili kwa kupata kura 3845 nafasi ya tatu akiwa Nathan Edward Mnyawami kwa kupata kura 1993 nafasi ya nne akiwa Festo John Kipate aliyepata kura 1352 watano ni Shamdi Sadro Nzogela ambaye amepata kura 1111 huku nafasi ya sita na ya mwisho akiwa Mwalubadu Riziki Ngaga aliyepata kura 317
Aidha katika jimbo hilo la Kilolo jumla ya idadi ya kura zilizopigwa zilikuwa 13,376 na kura zilizoharibika zilikuwa 250 huku idadi ya kura halali ikiwa ni 13,126.
Kwa upande wa jimbo la Mufindi Kusini dadi ya kura zilizopigwa zilikuwa ni 7,111 idadi ya kura zilizoharibika 78 na dadi ya kura halali zikiwa 7,033 ambapo matokeo yalionesha aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo David Mwakiposa Kihenzile alitabgazwa kuongoza katika kura za maoni akifuatiwa na Gasper Josephat Mwagala nafasi ya tatu ikiwa ni kwa Golden Ally Mgonzo Chavala Matonya Yohanes akishika nafasi ya nne huku Emmanuel Israel Ng'ahala akishika nafasi ya tano.
Tukiangazia jimbo la Mafinga mji Idadi ya kura zilizopigwa zilikuwa ni 2,684 kura zilizoharibika zilikuwa ni 38 na idadi ya kura halali ikiwa ni 2,646 na matokeo katika jimbo Dickson Lutevele Nathan alitangazwa kuongoza kwa kupata kura 1219 Agrey Naftary Tonga nafasi ya pili kwakuwa na kura 878 na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi akishika nafasi ya tatu kwakupata kura 376 nafasi ya nne akiwa ni Dr. Bazil Lwisijo Tweve aliyepata kura 129 huku aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mendrad Lutengano Kigola akipata kura 44.
Na Mufindi Kaskazini Idadi ya kura zilizopigwa 5,099 idadi ya kura zilizoharibika 60 huku idadi ya kura halali ikiwa ni 5,039 katika matokeo ya kura za maoni jimboni humo Abdulwahab Luqman Mehrab alipata kura 3,795 aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amepata kura 488 Pro. Obadia Venance Nyongole kapata kura 435, Godfrey William Ngupula akipata kura 186 na Alban Joseph Lutambi akishika nafasi ya tano aliyepata kura 135.
Wajumbe wamemaliza kazi yao kwa kupiga kura ya maoni ikiwa nikueleza kwa vitendo wanamtaka nani, lakini CCM inazitaja sifa hizi za uongozi kama muhimu kwenye kumtafuta mwakilishi wa chama hicho.
Hata hivyo, uamuzi wa wajumbe umetuma ujumbe mzito kwamba mabadiliko yanahitajika, na sura mpya zinaungwa mkono.
Kwa waliokuwa wabunge waliokataliwa na wanachama wao, matumaini pekee yaliyobaki ni uamuzi wa huruma kutoka juu kama utakuwepo.
Sasa hatua muhimu itakayofuata baada ya mchakato wa awali wa kura za maoni ni Kamati za Siasa kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Jimbo/Wilaya na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya.
IDADI YA WABUNGE WA MAJIMBO WALIOANGUKA .
Wabunge ambao kura hazikutosha kutetea nafasi zao ni pamoja na Costo Chumi mbunge wa Mafinga Mjini na naibu waziri wa mambo ya ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Exaud kigahe mbunge wa Mufindi Kaskazin ambae ni naibu waziri wa viwanda na Biashara
Jesca Msambatavangu mbunge wa jimbo la Iringa mjini .
0 Comments