Na Mwandishi Wetu.
Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bw. Ismail Laizer akitoa elimu kuhusu masuala ya viwango kwa wananchi waliohudhuria maonesho ya nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
TBS imewasisitiza wananchi kutotumia vipodizi vyenye viambata sumu kwa ajili ya usalama wa kiafya.
Katika maonesho ya kitaifa ya Nane Nane yanayofanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8, 2025, katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu muhimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya bidhaa, hasa vipodozi.
Afisa Udhibiti Ubora wa TBS, Bw. Ismail Laizer, aliwasisitiza wananchi kuepuka vipodozi vyenye viambata hatari kwa ajili ya kulinda afya zao na usalama wa ngozi na kuhakikisha wananunua vipodozi vilivyothibitishwa na TBS kwa ajili ya usalama wao .
Aidha aliongeza kuwa serikali kupitia TBS , inatoa alama ya ubora bure kwa wajasiriamali na wazalishaji wa bidhaa, lengo likiwa ni kuinua ubora wa bidhaa za Kitanzania sokoni.
Kupitia elimu hii, wananchi na wajasiriamali wamewezeshwa kufahamu umuhimu wa viwango bora katika uzalishaji na matumizi ya bidhaa za kila siku.
0 Comments