Header Ads Widget

JASMINE WEWE NI BINTI SHUJAA HONGERA UMEWAKILISHA VEMA IRINGA -SHALOM


Kada wa UVCCM Mufindi Shaloom Robert 

Kada wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM ) wilaya ya Mufindi Shalom Robert amempongeza mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ya Mufindi Jasmin Ng'umbi kwa kuwakilisha mkoa wa Iringa kwenye mchakato wa kura za maoni   nafasi ya ubunge vijana Taifa .

kuwa uamuzi huo ni mkubwa na ni uthubutu wa kiwango cha juu ambao vijana Mufindi na mkoa wa Iringa wanampongeza hasa jina lake liliporejeshwa na kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa iliyoongozwa na mwenyekiti CCM Taifa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

"Hongera sana Jasmine Chesco Ng’umbi,binti wa kitanzania kutoka ardhi ya Mkwawa umeonyesha uwezo mkubwa na dhamira ya kulitumikia taifa lako kupitia vijana,hakika umekuwa daraja kwa vijana hasa mabinti wa kike wenye ndoto za kisiasa"

Alisema kuwa Jasmine ni matumaini yangu kuwa si wewe uliyeenda kuomba ridhaa ya kuwatumikia vijana katika bunge la Tanzania bali ni vijana wenyewe waliokutuma na hii imeleta heshma kubwa kwa mkoa wetu wa Iringa kwani umeonyesha uwezo mkubwa katika kufikisha ujumbe na malengo uliyonayo juu ya vijana na hapa nitakuita wewe ni “BINTI SHUJAA”.

kuwa Mwisho wa safari ni mwanzo wa safari nyingine na hapa ni imani yangu kuwa umefungua njia ya safari nyingine mpya ya kisiasa.

Sholom alisema Vijana wanamtazama ,vijana wanaimani Jasmin kwani  vijana wanataka akawatumikie.

"Huu mwema wa safari basi ianze safari hii kwa ujasiri tena na uisimamie imani waliyokupa vijana hawa wa kitanzania"


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI