Header Ads Widget

CCM KUTANGAZA WAGOMBEA AGOSTI 23.

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

DODOMA - Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza ratiba ya vikao vyake vya kitaifa vitakavyofanyika jijini Dodoma kuanzia Agosti 21, 2025 chini ya Mwenyekiti wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA. Amos Makalla, kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) kitafanyika Agosti 21, kikifuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kitakachofanyika Agosti 23.

Ajenda kuu ya vikao hivyo ni kufanya uteuzi wa wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na wajumbe wa Viti Maalum vya Baraza la Wawakilishi.

Vikao hivyo vinatarajiwa kuvuta hisia kubwa kutoka kwa wanachama na wananchi kwa ujumla, hasa ikizingatiwa kuwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI