Header Ads Widget

WASICHANA 2300 KUNUFAIKA NA URASIMISHAJI UJUZI KIGOMA

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ENABEL Koen Geokint

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shirika la Ushirikiano wa kimataifa la serikali ya Ubelgiji linatarajia kutumia Zaidi ya  shilingi Bilioni tatu kurasimisha ujuzi kwa wasichana 2300 mkoani Kigoma ili ujuzi wao uweze kutambuliwa kwenye mifumo ya ajira na kazi mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Enabel Koenrad Goekint alisema hayo katika mahafali ya kwanza ya wanafunzi 112 waliorasimisha ujuzi wao na wanafunzi 45 wanasomea ujenzi wa madaraja ya mawe wanaosomeshwa na Shirika la ENABEL katika chuo cha VETA Kigoma.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wasichana hao kuendana na soko la ajira kwa kuajiriwa au kujiajiri kwa kupata mikopo na uwezeshaji kutoka taasisi za fedha kutokana na ujuzi walioupata kutambuliwa na mamlaka mbalimbali.

mradi umelenga  kuwezesha wasichana wenye 2300 umri wa kati ya miaka 17 hadi 28 kupata ujuzi katika vyuo vya ufundi stadi mkoani Kigoma.

Akihitimiza mafunzo hayo katika mahafali yaliyofanyika chuo cha VETA Kigoma WAZIRI wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake  na makundi Maalum Dk.Doroth Gwajima amewataka wanafunzi wasichana waliohitimu mafunzo ya uanagenzi kutoka Chuo cha ufundi Stadi (VETA) kutumia ujuzi wao kuanzisha shughuli za kiuchumi badala ya kukimbilia kwenye mahusiano na wanaume na kuwa tegemezi.

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI