Header Ads Widget

WAKAMATWA NA VIUNGO VYA BINADAMU KAGERA.

 

Na Shemsa Mussa -Matukio daima.   

               Kagera 

JESHI  la polisi mkoani Kagera linawashikiria watuhumiwa Kelvin Wawili, Mdolo(42) na Randeni Seme(64)wakazi wa Mkoa wa Songwe kwa kupatiakana na viungo vinavyodhaniwa  kuwa ni viungo vya binadamu.

Akithibitisha kukamatwa kwa tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kagera Brasius Chatanda amesema June 17mwaka huu 2025 Kelvin Mdolo alikamatwa akiwa na viungo vya binadamu akiwa katika nyumba ya kulala wageni.

Aidha alisema mtuhumiwa alikuwa na mfupa wa taya,kipande cha moyo,sehemu za Siri za mwanamke, ,kondo la nyuma la uzazi,vipande viwili vya ngozi vilivyokaushwa vidhaniwavyo ni vya nyoka aina ya chatu.

Aliendelea kutaja kuwa pembe mbili za mnyama wa polini na vipande vitatu vya mifupa ambavyo havija tambulika kuwa ni mnyama au binadami.

Aliongeza kuwa vitu hivyo  alitumia katika uganga wa  jadi  na kupiga ramli chongamishi katika mahali ambapo alikuwa akiishi baada ya kufika mjini Bukoba.

Alisema baada ya kumfikisha katika kituo cha polisi na kufanya mahojiano mtuhumiwa alimtaja aliyempatia  vitu hivyo aitwaye Randani Seme Mlomo ndiye aliyempatia  viungo akiwa wilaya ya mbozi mkoani Songwe.

Hata hivyo alisema mtuhumiwa wa pili ambaye ni Randani Seme alikuwa mfanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Vwawa wilayani Songwe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI