Header Ads Widget

SHAMBULIZI LA NYUKI LAWAACHA WATATU KATIKA HALI MBAYA NA MAKUMI WAKIJERUHIWA

 

Watu watatu katika mji mmoja huko Ufaransa wako katika "hali mbaya" kufuatia kushambuliwa na nyuki mwishoni mwa juma na pia kusababisha wapita njia 24 kujeruhiwa, amesema Meya wa mji wa Aurillac, siku ya Jumatatu.

Watu 24 walijeruhiwa na watatu walikimbizwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya pale mamia ya nyuki waliposhambulia ghafla watu katika mji wa kati-kusini siku ya Jumapili asubuhi.

Kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo, mmoja wao alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 78 ambaye aliumwa mara 25 na ilibidi azinduliwe baada ya kupoteza fahamu kwa mshituko wa moyo.

Polisi na zima moto walizingira eneo hilo na mfugaji nyuki aliitwa ili kuwatia moshi nyuki hao - njia salama ya kutuliza wadudu hao.

Meya wa Aurillac, Pierre Mathonier, aliripotiwa akisema wadudu aina ya nyigu wanaotishia mzinga wa nyuki wanaweza kuwa ndio sababu ya shambulio hilo.

Lakini Christian Carrier, rais wa muungano wa wafugaji nyuki, ana mashaka na madai hayo. Aliiambia France Info, nyuki kwa ujumla huepuka kuondoka kwenye mizinga yao pakiwa na wadudu nyigu.

Badala yake, alisema tukio hilo lisilo la kawaida huenda lilitokana na kundi la nyuki kuwa kubwa katika mzinga wake na kutawanyika wakati mfugaji nyuki alipokuwa akishughulika na mzinga huo.

"Huenda [nyuki] hawakuwa na nafasi ya kutosha katika mzinga na hawakuwa na nia ya kuondoka. Hilo linaweza kusababisha nyuki kuwa wakali," amesema Carrier.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI