NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,MUFINDI
MKUU wa mkoa wa Iringa Kheri James amepongeza jitihada mbali mbali zinzofanywa na watumishi wa Halmashauri Mufindi kwa kazi nzuri inayofanywa huku akitaka kuongeza nguvu kubuni vyanzo vya mapato.
kuwa Halmashauri ya Mufindi imekuwa ikifanywa vema katika makusanyo ya mapato hivyo kuna kila sababu ya Halmashauri hiyo kupngeza nguvu zaidi katika kukusanya mapato .
Akizungumza na watumisha wa Halmashauri hiyo leo wakati wa kikao chake kwa kujitambulisha na kufahamiana zaidi toka alipoteuliwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa ni vizuri watumishi hao kutumia vizuri kiapo chao cha utumishi wa umma katika kuwatumikia wananchi na serikali badala ya kufanya kazi kwa mazoea na kuamini kuwa kazi hiyo ndio mwisho wa kazi tena.
"Wapo baadhi ya watumishi wanabuni mbinu mpya ya kutengeneza mifumo yao kwa ajili ya kujipatia fedha zisizo sahii huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyime na maadili na ni uhujumu uchumi hivyo wanapaswa kuachana na mchezo huo "
Alisema kwa sasa amekuja kwa ajili ya kutoa elimu kwani kiongozi mzuri ni yule anayeanza na kufundisha kisha kuja kuhukumu badala ya kuhukumu badala ya kufundishana.
Hivyo alisema lazima kila mmoja kuhakikisha anatumia vizuri nafasi yake kwa maslahi mapana ya jamii.
Alisema kuwa shauku kubwa ya wananchi ni kuendelea kuona makusanyo yao yanatumika kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.
Hata hivyo alisema ili Halmashauri iweze kujiendesha ni lazima kuweka mpango wa kukusanya .
Alisema kuwa kwa makisio waliyojiwekea ya kukuanya kiasi shilingi bilioni 104 na kiasi cha shilingi bilioni 86 kwa ajili ya fedha za miradi ya maendeleo ili kufanikiwa lazima kuwa na mipango kabambe ya kufikia malengo ya makusanyo.
Kheri alimtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi kuendelea kufanya kazi kwa kukaza minya ya wapigaji ili kufikia malengo ya serikali katika kuwahudumia wananchi katika miradi ya maendeleo .
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kilio chake kwa Mufindi ni mapato hivyo lazima kuhakikisha wanaongeza nguvu katika mapato na dosari kidogo kuzifanyia kazi .
Alisema kuwa leo amekuja kama mwalimu na wakati mwingine atakuja kama hakimu japo kwa kazi nzuri ya Halmashauri hiyo hakuna utata wa kutuma wachunguzi ama taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguzi.
Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa aliwataka watumishi hao kuwa na mahusiano bora ili kuja kufanikiwa katika mipango mbali mbali .
Alisema mahusiano bora ni pamoja na ushirikiano mzuri kati ya mtumishi na mtumishi isiwe kila mmoja anafanyakazi kwa kujitenga .
kuwa mahusiano mabovu ni pamoja na kuacha kumkadilia mkuu wa idara kwa umbo ama kipato chake bali kuheshimu mamlaka wakati wote badala ya kumkadilia kwa uchumi ama umri au kitu chochote kile kwani mtu ukimletea dharau atakuacha na utaharibikiwa.
Pia ataka maafisa utumishi katika Halmashauri zote kuhakikisha wanawatendea haki watumishi wanaowaongoza wale wanaohitaji haki zao kupewa kwa wakati badala ya kuzungushwa.
Alisema kuwa utumishi wa umma ni kuhitajiana hivyo unsyemfanyia ndivyo sivyo leo kesho utahitaji msaada wake.
Kuwa kauli mbiu yetu baada ya ile ya jamhuri ya muungano wa Tanzania itafuata hii Iringa imara tutaijenga kwa umoja na uwajibikaji
0 Comments