Wafanyakazi wa shamba walijeruhiwa vibaya baada ya uvamizi wa wahamiaji katika shamba la kukuza bangi huko California, ambapo takriban watu 200 - ikiwa ni pamoja na watoto 10 - waliwekwa kizuizini, kulingana na chama cha wafanyakazi.
"UFW inaweza kuthibitisha kuwa wafanyakazi wa mashambani walijeruhiwa vibaya jana wakati wa msako mkali katika Kaunti ya Ventura, California. Wengine, ikiwa ni pamoja na raia wa Marekani ambao bado hawajulikani waliko," Chama cha United Farm Workers kilisema katika taarifa Ijumaa usiku.
Chama hicho kiliripoti kifo kimoja kati ya wafanyikazi lakini baadaye kilisema kifo hicho hakikuthibitishwa.
Mapigano yalizuka nje ya shamba la Glass House huko Camarillo siku ya Alhamisi huku wafanyakazi wakikabiliana na maafisa wa usalama katika jaribio la kusimamisha uvamizi huo.
Mabomu ya machozi yalirushwa dhidi ya wafanyakazi na askari wa Ulinzi wa Kitaifa wakiwa na bunduki na barakoa za kujikinga wakijaribu kuwazuia kuingia kwenye eneo la ndani la shamba.
Inasemekana kuwa mtu mmoja aliwafyatulia kitu kama bastola maafisa wa usalama.
Haijulikani ni wapi vijana hao wanatoka, lakini Mkuu wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka Rodney Scott alisema aliyekuwa na umri mdogo ni miaka 14.
Maafisa wa usalama "waliokoa takriban watoto 10 wahamiaji kutoka kwa kile kinachoonekana kama dhulma, ajira ya watoto kwa kulazimishwa, na uwezekano wa biashara ya usafirishaji wa binadamu au kuingizwa kimagendo," Katibu Msaidizi wa Idara ya Usalama wa Nchi Tricia McLaughlin alisema katika taarifa.
Bangi ni halali na inadhibitiwa huko California – uvamizi huu ulihusisha wafanyikazi, sio bidhaa.
0 Comments