Header Ads Widget

MKE WA DIOGO JOTA AANDIKA MTANDAONI "NI WANGU MILELE"

 Mke wa mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota ameadhimisha mwezi wa kwanza wa ndoa yao, wiki tatu baada ya Jota kufariki katika ajali ya gari.

Rute Cardoso aliweka picha za harusi yao iliyofanyika Juni 22, katika akaunti yake ya Instagram.

Picha tatu ziliambatanishwa na maneno "mwezi mmoja wa 'hadi kifo kitakapotutenganisha," na kuongeza kuwa "ni wangu milele".

Jota, 28, alifariki dunia tarehe 3 Julai wakati gari aina ya Lamborghini alilokuwa akisafiria na mdogo wake, Andre Silva, lilipotoka tairi likapinduka na kuwaka moto huko Cernadilla katika jimbo la Zamora nchini Uhispania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI