Header Ads Widget

MIRADI MIKUBWA KUJENGWA KAGERA.


Na Shemsa Mussa -Matukio Daima 

                     Kagera.

Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, imetia saini Mikataba minne ya ujenzi wa miradi mikubwa ya stendi ya mabasi, soko kuu, kingo za mto kanoni na barabara kilometa 10.7 kwa thamani ya shilingi bilioni 40.2 kwa ufadhili wa benki ya dunia kupitia mradi wa TACTICS.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba hiyo Mkuu  wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa, amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi ndani ya Mkoa huo  pamoja na kupendezesha mji na kuwataka wakandarasi watakao tekeleza miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa  Kagera amewataka wananchi wa manispaa ya Bukoba pamoja na mkoa kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa wakandarasi na kuwa walinzi wa miradi hiyo wakati wa utekelezaji wake.

Awali akisoma taarifa ya miradi hiyo meneja wa wakala barabara mjini na vijiji TARURA wilaya ya Bukoba mhandisi Emmanuel Festo Yohana, ameeleza kuwa miradi hiyo imegawanyika katika makundi mawili stendi ya mabasi na soko kuu vitajengwa kwa shilingi bilioni 18.95 na ujenzi wa Barabara na taa za Barabarani pamoja na kingo za mto kanoni kwa shilingi bilioni 21.29. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI