Header Ads Widget

WAANDAMANAJI WAJITOKEZA WAKIDAI HAKI KWA ALBERT OJWANG

Waandamanji wamejitokeza katika jiji la Nairobi nchini Kenya, wakiimba nyimbo zinazosema ‘Ruto Must Go’ huku baadhi ya mabango walioshika yakiwa na maneno yanayotaka Naibu Inspekta wa Polisi ajiuzulu.

Waandamanaji hao ambao pia wameshika bendera za Kenya, wamevaa fulana zenye picha za Ojwang, kijana aliyekufa akiwa amezuiliwa pamoja na watu wengine waliouawa na polisi.

"Lagat anapaswa kujiuzulu, sio kujiondoa", moja ya bango lilikuwa likisomeka hivyo.

Hata hivyo, wakati waandamanaji walipokuwa wameanza maandamano yao ya amani, ghafla kulionekana msururu wa pikipiki zilizoshukiwa kuwa wahuni waliojipanga kuingilia maandamano hayo na kuanza kuvamia waandamanaji.

Inadaiwa waandamanaji walipandwa na hasira na kumvamia mmoja wa waliokuwa kwenye msafara wa pikipiki na kuanza kumshambulia.

Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Eliud Lagat aliondoka kwenye cheo chake kupisha uchunguzi unaoendelea kwa sababu ya kifo cha Albert Ojwang, mwanablogu aliyekufa mikononi mwa polisi.

Katika taarifa iliyotolewa Juni 16, 2025, Lagat alisema amechukua hatua hiyo kwa nia njema kutokana na jukumu na wajibu alionao kwenye nafasi yake.

Lagat aliongeza kuwa majukumu yake yatatekelezwa na naibu wake hadi uchunguzi utakapokamilika.

Mamlaka huru ya uangalizi wa polisi (IPOA) imethibitisha kwamba Albert Ojwang alikufa ndani ya seli ya polisi, madai ambayo yalikinzana na taarifa iliyokuwa imetolewa awali, kwamba mwanablogu huyo alijiua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI