Header Ads Widget

RAIS AKUBALI OMBI LA PETER SERUKAMBA KWENDA KUTIA NIA UBUNGE

TAZAMA VIDEO YAKE AKITANGAZA KUACHA UKUU WA MKOA
 Zimepita wiki chache toka Peter Serukamba kutangaza kwenda kutia nia ubunge mkoani Kigoma na kuandika barua kwa mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuomba kuruhusiwa kwenda kwenye ubunge.

kupitia kikao cha Halmashauri kuu maalum ya CCM mkoa wa Iringa kilichofanyika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti Daud Yassin ,Serukamba mbali ya kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM pia aliaga rasmi nafasi yake ya ukuu wa mkoa kuwa anatamani kuwa mbunge .

Leo majibu rasmi yametoka ya kukubaliwa kwenda kutia nia ubunge kupitia CCM ambayo ni safari ya matumaini .

Kwa kuwa safari ni hatua CCM mkoa wa Iringa kiliweza kumpa baraka zote na kwa kuwa leo rasmi ameondolewa kwenye nafasi yake ni wazi atakwenda kujiandaa vilivyo.


kuna mambo ya kujifunza kwake ambayo Iringa itamkumbuka pia kuna mambo ya yeye amejifunza kwa mkoa wa Iringa ila leo itoshe kusema kila lakheri kwake ipo siku nitasema zaidi .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI