Header Ads Widget

NJEZA ATEKELEZA AHADI YA GENERATOR KANISA RC ILEMBO.

 


Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, amekabidhi Generator lenye thamani ya shilingi laki nane kwa uongozi wa kanisa la Mtakatifu Yakobo mtume Parokia ya Ilembo kwa ajili ya waimbaji wa kwaya za Familia Takatifu na kwaya ya Mtakatifu Agustino.


Hii ni kwa ajili ya kwaya hizo zinapoenda kuhubiri katika maeneo mbalimbali na kanisa kwa ujumla kama walivyoahidiwa na Mbunge Njeza baada ya kumuomba msaada wake miezi miwili iliyopita ambapo pia aliwanunulia na kuwakabidhi kinanda cha kisasa.


Pamoja na hayo Mhe. Mbunge Oran Njeza amekabidhi mchango wake wa shilingi laki tano kwa ajili ya shughuli ya upadirisho wa mtumishi wa MUNGU Eneliko Mwamwezi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2025 katika kanisa la Roman Catholic Parokia ya Ilembo.



Mchango na sadaka hiyo kwa kanisa umekabidhiwa kwa niaba yake na katibu wake Peter Mtepa na kupokelewa na wanakwaya wakiongozwa na paroko wa Parokia hiyo Padri Stephano Gindo.



Mtepa akizungumza na mamia ya waumini wa kanisa hilo amesema huo ni mwendelezo wa Mhe. Mbunge kutekeleza ahadi ambayo walimwomba alipofanya ziara katani humo (Ilembo) kama ambavyo amekuwa akitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo kwenye nyumba za ibada jimboni kwake.


Paroko wa Parokia ya Ilembo Stephano Gindo, amemshukuru Mbunge kwa kuwa na moyo wa upendo na kujali watu wake na kuchangia sadaka kwa ajili ya upadirisho huku nao waimbaji wakiahidi kumwombea kwa Mungu kiongozi huyo kwa mchango wake katika kuinua uinjilishaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI