Na,Jusline Marco;Arusha
Katika kuhakikisha utoaji huduma unakuwa bora, Serikali ya awamu ya sita imehakikisha upatikanaji wa huduma hizo unakuwa karibu na wananchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ameyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Madaktari nchini na Maadhimisho ya miaka 60 ya Chama cha madaktari Tanzania unaofanyika jijini Arusha.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa katika kutumiza azma hiyoo serikali imejenga vituo vya afya,hospitali za halmashauri,hospitali za wilaya na mikoa ili kuwafanya wananchi kupata huduma za afya kwenye maeneo yao ya karibu.
Aidha amesema ongezeko la maeneo ya kutolea huduma limewezesha asilimia 80 ya watanzania kupata huduma kwa ukaribu katika umbali mdogo chini ya kilomita tano.
Kwa upande wake rais wa Chama cha Madaktari nchini Dkt. Mugisha Nkoronko katika mkutano huo amesema moja ya changamoto inayowakabili madaktari nchini ni uongezaji wa misharaha kulingana na kiwango cha elimu aliyonayo daktari ambapo ameiomba serikali kuangalia upya suala hiyo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema Mkoa wa Arussha umepiga hatua katika sekta ya afya kutoka kilometa 15 hadikufikia kilometa 4 kwa kuongeza zaidi ya vituo 75 vilizogharimu shilingi bilioni 90 ambazo zimejumuisha vifaa,ujengaji wa majengo pamoja na uongezaji wa wataalam kwenye sekta zote ndani ya sekta ya afya.
0 Comments