Header Ads Widget

MCH HANANJA "PIGA PINI MAKANISA YOTE YANAYOKIUKA UTARATIBU"

 

Na Fatma Ally Matukio DaimaApp

Mchungaji mstaafu wa hiari na Mkurugenzi wa Taasisi ya Hananja Compassion foundation inayohusika na watu wanaotumia dawa za kulevya, Richard Hananja ameitaka Serikali kuyafungia makanisa yote ambayo yanakiuka sheria na utaratibu uliowekwa wakati wa usajili ili kuifanya nchi iendelee kuwa na amani.

Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizungimza na waandishi wa habari ambapo amesema kumekuwepo na makanisa mengi ambayo hayafuati utaratibu hali ambayo inaleta taharuki ndani ya jamii.

Amesema kuwa, hapingi mawazo yanayotolewa na watu lakini kumekuwa na utaratibu mbovu unaotumiwa na viongozi wa dini ambao wamekua wakitumia mazabau yao vibaya kwa kuwatukana viongozi wa Serikali kuwatolea maneno ya kashfa na kuwazomea.

"Kwani haya mambo ya utekaji yameanza leo, kwa nini wajitokeze sasa, jiepusheni kuingilia mambo ambayo ni maslahi ya watu, wameona uchaguzi umekaribia ndio wanajitokeza, wanataka kutuvuruga "amesema Mchungaji Hananja. 

Aidha, amesema Mnec ana nafasi ya kubwa ya kuonana na Rais na kumueleza jambo lolote ambalo anaona halitojitokeza sawa kwa taifa na sio kutumia mazabau kwenda kumtukana au kumzomea, 

Ameongeza kuwa, hakuna nchi ambayo imetulia duniani, ni vyema watu wakakosoa kwa uvumilivu, kama kuna sehemu ambayo watu wanaona mambo hayaendi sawa ni vizuri kukosoa kwa kuvumiliana, na sio kutumia lugha za matusi jambo ambalo si sahihi. 

"Viongozi wa dini mnaoshabikia mambo haya nyote mtapata hasara hakuna kiongozi ambae atabaki salama nchi ikiingia kwenye machafuko, tuilinde amani yetu kwa gharama yoyote ile"amesema Mchungaji Hananja.

Sambamba na hilo, amewataka watanzania kushiriki uchaguzi kikamilifu na kuchagua viongozi ambao ni sahihi na kuacha kuleta taharuki  kwa kusambaza taarifa ambazo si za kweli.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI