Header Ads Widget

MBUNGE PROF MUHONGO KUANIKA MAFANIKIO UTEKELEZAJI WA ILANI 2020/2025 KESHO


Na Shomari Binda-Musoma 

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof.Sospeter Muhongo kesho juni 20,2025 atasoma taarifa ya utekeleza wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020/2025


Utekelezaji huo utasomwa kubainisha mambo yaliyofanywa kwenye jimbo la Musoma Vijijini kwenye Mkutano Mkuu maalum utakaofanyika Kata ya Murangi.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge huyo imesema jumla ya wajumbe 2,554 na wageni 30 watashiriki mkutano huo.


Taarifa hiyo imesema yapo mambo mengi ambayo yametekelezwa kupitia ilani inayomalizika ambayo yametekelezwa kuanzia elimu,afya,maji,miundombinu na masuala ya kijamii.


Licha ya kusomewa taarifa hiyo wajumbe na waalikwa wa mkutano huo watapata vitabu vinavyoelezea utekelezaji huo ndani ya jimbo la Musoma Vijijini.


" Lengo la Mkutano Mkuu huu maalum ni mbunge kuelezea mafanikio yaliyopatika kwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano (2020 - 2025)


"Wajumbe 2 ,554

wageni wa mbunge 30 watashiriki mkutano huo utakaopambwa na vikundi vya burudani mbalimbali kutoka ndani ya jimbo hilo",imesema taarifa hiyo.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya kichama ya Musoma vijijini Denis Ekwabi (Ruto)ambaye ataendesha mkutano huo amesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kila mjumbe ameshafikishiwa taarifa.


Mkutano mkuu huo umetanguliwa na kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo na Mkutano Mkuu maalum uliofanyika juni 18,2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI