Na Shomari Binda-Musoma
Wazazi kwenye familia wametakiwa kutatua migogoro ya kifamilia pale inapojitokeza ili kujiepusha kutengana na watoto kukosa malezi bora.
Hayo yamesemwa na diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Meryciana Masasi leo mei 15,2025 alipozungumza na Matukio Daima ikiwa ni siku ya familia duniani.
Amesema wimbi la watoto wa mitaani linazalishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na migogoro inayojitokeza kwenye familia.
Diwani huyo amesema iwapo migogoro inapojitokeza na kushindwa kusuruhishwa upelekea wazazi kutengana na watoto kukosa malezi hivyo kukimbilia mitaani.
Amesema watoto kukosa malezi ya pande mbili huwa kunatokea changamoto ya kimalezi na kushauri kuwepo na utatuzi wa migogoro ili kuepusha tatizo hilo.
" Kupitia siku hii ya familia duniani nitoe ushauri kwa wazazi kuwa na utaratibu wa utatuzi wa migogoro ili tuwalee watoto wetu kwa pamoja na kujenga familia.
" Watoto hatupendi waangaike mitaani na wanakuwa wanapata tabu na hii kwa asilimia kubwa inatokana na wazazi kutengana hivyo ni muhimu kuwa na utaratibu wa utatuzi wa migogoro",amesema.
Akizungumziawanawake kwenye familia amesema wana mchango mkubwa katika kusimamia nyumba na kudai wasiwe wepesi kukubali familia kutengana.
Ameongeza kuwa malezi ya Mama peke yake "single mother" sio mazuri na wasione ufahari kuitwa au kujiita jina hilo.
Kila ifikapo mei 15 kila mwaka duniani inaadhimisha siku ya familia huku ujumbe ukiwa unatolewa wa familia kuwa pamoja.
0 Comments