Takribani watu tisa wamefariki na wengine 70 wamelazwa hospitalini baada ya upepo mkali kusababisha boti nne za watalii kupinduka kusini magharibi mwa China.
Upepo mkali wa ghafla ulisababisha boti hizo kupinduka kwenye mto katika mji wa Qianxi huko Guizhou siku ya Jumapili, na kusababisha watu 84 kutumbukia majini, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya serikali.
Zaidi ya watu kumi na wawili walikuwa hawajulikani walipo, lakini wote isipokuwa mmoja sasa wameokolewa.
Tukio hilo lilitokea wakati China ikisherehekea mwisho wa likizo yake ya wiki ya Mei Mosi, msimu wa kilele wa kusafiri.
Kiongozi wa China Xi Jinping hapo awali alihimiza "juhudi" katika utafutaji na uokoaji.
Tukio la Jumapili linakuja miezi miwili tu baada ya watu 11 kupoteza maisha katika ajali nyingine, wakati boti ya abiria ilipogonga meli ya viwandani katika mkoa wa Hunan nchini China.
Ajali nyingine ilitokea mwishoni mwa juma katika mji wa mashariki wa Suzhou, baada ya helikopta ya kitalii kuanguka katika bustani iliyofunguliwa hivi karibuni na kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wanne waliokuwa ndani yake.
0 Comments