Header Ads Widget

UWT MARA YAWATAKA WANAWAKE MUSOMA MJINI KUSEMEA MAZURI YALIYOFANYWA NA RAIS DKT.SAMIA

 

Na Shomari Binda-Musoma 

KATIBU wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM ( UWT) mkoa wa Mara Saadan Mwamba amewapa ujumbe wanawake wa Musoma mjini kumsemea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi nzuri anayoifanya

Ujumbe huo ameutoa leo mei 18,2025 kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara alipokuwa akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi ya matawi na Kata pamoja na madiwani wa viti maalum ikiwa ni muendelezo wa ziara kwenye Wilaya.

Amesema Rais Dkt.Samia amefanya kazi kubwa katika kuwaletea maendeleo wananchi ambayo wengi walikuwa hawategemei hivyo lazima wazisemee.

Katibu huyo ambaye ameambata na wajumbe wa Kamati Tekelezaji ya UWT mkoa wa Mara amesema Rais Samia amegusa sekta zote kuanzia elimu,afya,maji,miundumbinu na masuala ya uchumi na cha kumlipa ni kumchagua kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Amesema miaka 4 ya uongozi wake hakuna mzazi alichangishwa fedha shuleni shule mpya zikijengwa na kuongezwa kwa madarasa hali inayowafanya wanafunzi kusoma karibu na nyumbani.


Katika sulala maji Saadan amesema mwanamke ametuliwa ndoo kichwani mjini na vijijini huku kwenhe afya zahanati,vituo vya afya na hospitali zimejengwa kila mahala.

" Ndugu zangu wanawake wa Musoma mjini kwa mambo makubwa ambayo ameyafanya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tutembee kifua mbele na twendeni tukamsemee.


" Tukafanye ziara kuanzia ngazi ya mashina tumsemee na muda ukifika shukrani yake ni kumpa kura nyingi za kishindo na watakaotoa kura nyingi tutakutana kwenye ukumbi huu baada ya uchaguzi kupeana zawadi"amesema.

Akizungumzia uhai wa jumuiya na chama amesema ni muhimu kulipa ada na kufanya ziara ngazi zote huku akisisitiza kupendana na kuepuka kutengenezeana ajali za kisiasa.

Aidha Katibu Saadan ameelezea mabadiliko ya kanuni za UWT zilizotolewa chini ya chama ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa wajumbe kwenye vikao vya maamuzi.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Musoma mjini Teddy Mageni ameseema wataendelea kufanya kazi za jumuiya na chama kama maagizo ya mkoa yalivyotolewa.

Teddy amemuhakikishia Katibu wa UWT mkoa wa Mara ziara zitafanyika na kuzingatia maagizo na maelekezo yote yaliyotolewa

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI