NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MRADI wa Ujenzi wa Daraja jipya la Rau madukani-Mamboleo-Materuni umekamilika ambapo imeondoa hadha kwa wananchi.
Daraja hilo limekua kiunganishi muhimu kwa nyanja za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wanaoishi katika kata hizo na kata jirani ambapo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 910 zilizotolewa na serikali.
Wakizungumzia ujenzi huo Wananchi hao, Anna Temba alisema kuwa awali walikuwa wakipata changamoto kubwa hasa kipindi cha mvua kupita katika eneo hilo.
Alisema kuwa, wakati mwingine walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kuzunguka lakini kukamilika kwake kutasaidia kuinua uchumi wa maeneo hayo.
Naye Arnold Mushi aliishukuru Serikali kwa kufadhili mradi huu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Uru Mashariki, Samwel Materu, pamoja na Diwani wa kata ya Uru Shimbwe, Bertin Mkami kwa kuupigania mradi huo.
Mwisho.
0 Comments