Header Ads Widget

TAZAMA ZIARA YA OTHMAN MASOUD AKIELEKEA KUJENGA CHAMA CHA ACT WAZALENDO TUMBATU


NA MATUKIO DAIMA MEDIA ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman ameanza ziara ya uimarishaji wa Chama kisiwani Tumbatu Mkoa wa kaskazini Unguja kwa ajili ya kujipangia na ushindi katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.

Ziara hiyo imekuja kufuatia mwendelezo wa ziara za visiwa alioanzia Kisiwapanza Mkoa wa Mkoani Pemba.


Mara baada ya kuwasili kisiwani Tumbatu (Jongowe) viongozi mbali mbali wa Chama na wazee mashuhuri wa kisiwani hicho walifika na kumpokea.


Akiwa eneo hilo la Jongowe alipata nafasi ya kuweka jiwe la msingi tawi la Chama na kuahidi kumalizia uwezekaji wa jengo hilo.


"Kwa hatua hii muliofikia hongereni sana na mimi nikiwa Mwenyekiti wenu naahidi kumaliza uezekaji ili kuimarisha Chama kuchukua ushindi uchaguzi wa mwezi Oktoba" alisema.


Katika hatua nyengine Othmana ambae ni Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar amesema kuna umuhimu mkubwa wa uimarishaji wa majengo ya Chama kwa kuwa ndio sehemu sahihi ya kufanya shughuli za siasa ambazo zinalenga kudai mabadikiko ya kiongozi.


Awali Naibu katibu mkuu wa Chama hicho Omar Ali Shehe amesema ujenzi wa matawi ya Chama na uimarishwaji umekua ukifanyika kila mahala na kuwataka wananchi kujitolea kuimarisha Chama chao.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI