Header Ads Widget

RAIS KIM ASHUTUMU KUHUSU 'AJALI MBAYA' WAKATI WA UZINDUZI WA MELI YA KIVITA KOREA KASKAZINI

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amelaani "ajali mbaya" wakati wa uzinduzi wa meli mpya ya kivita siku ya Alhamisi, na kuiita "kitendo cha uhalifu" ambacho hakiwezi kuvumiliwa.

Sehemu ya chini ya meli hiyo yenye uwezo wa kuangamiza tani 5,000 iliharibiwa, na hivyo kusababisha meli kukosa usawa, vyombo vya habari vya serikali viliripoti.

Kim ambaye alikuwepo kwenye uzinduzi huo, ameagiza kurejeshwa kwa meli hiyo kabla ya mkutano mkuu wa chama utakaofanyika mwezi Juni, na kwa wale waliohusika kutengeneza meli hiyo wawajibishwe kwa tukio hilo ambalo alisema "liliharibu sana heshima na fahari ya taifa letu kwa papo hapo."

Vyombo vya habari vya serikali havikutaja majeruhi au majeraha yoyote kutokana na tukio hilo.

Aliongeza kuwa "makosa ya kutowajibika" ya wale waliohusika yatashughulikiwa katika mkutano wa jumla mwezi ujao.

Haijabainika ni adhabu gani wanaweza kukabiliwa nayo lakini serikali ya kimabavu ina rekodi mbaya ya haki za binadamu.

Sio kawaida kwa Korea Kaskazini kufichua hadharani ajali za ndani - ingawa imefanya hivi mara kadhaa huko nyuma.

Novemba mwaka jana, ilielezea mlipuko wa angani wa satelaiti ya kijeshi miezi sita mapema kama "ushindi mkubwa" na ilikosoa maafisa ambao "walifanya matayarisho bila kuwajibika" kwa hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI