NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini, Afrey Nsomba, ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Kata ya Mbarizi Road kilicholenga kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika ngazi ya kata.
Katika kikao hicho, kilichowakutanisha viongozi wa chama na serikali kutoka ngazi ya msingi hadi kata, Mwenyekiti Nsomba aliwahimiza viongozi wa chama kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akisisitiza mshikamano na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi.
Amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM ni kipimo muhimu cha utendaji wa viongozi wa chama na serikali, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha ahadi za chama kwa wananchi zinatekelezwa kwa vitendo.
Kwa upande wao, wajumbe wa halmashauri kuu ya kata hiyo walieleza mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na chama katika kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma bora.
0 Comments