Header Ads Widget

MWENYEKITI CCM WILAYA YA HANDENI ANAVYOTUMIKA NA MBUNGE WA JIMBO LA HANDENI MJINI KUWATISHA WANACHAMA WA CCM HANDENI MJINI.

 


NA MWANDISHI WETU.


WAKATI  siku za Wabunge kuendelea kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao Bungeni zikihesabika, joto limezidi kuwa kali kwa baadhi ya  Wabunge hao baada ya  kuwa na wasiwasi na  hatima yao na uhakika wa kurejea Bungeni. 


Hatua hii inapelekea baadhi ya Wabunge wasiokubalika katika majimbo   yao kwa kutofanya  kazi  za kuridhisha  nakuwa na  mahusiano mabaya na wananchi  katika  miaka mitano tangu walipochaguliwa na sasa kuwatafuta viongozi wa chama kwa gharama kubwa  wawabebeshe mzigo wa lawama  ili kuona uwezekano wa kuwadanganya tena wananchi   wawachaguwe na kurejea mjengoni. 


Jimbo la Handeni mjini mkoani Tanga ni jimbo linaloongozwa na Mbunge Reuben Mtahamanilo Kwagilwa (CCM).


Mbunge huyo baada ya kuona hatima yake kuwa ndogo sasa ameanza kumtumia Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni, Amiri Changogo na mwenezi wa wilaya, Mkobe kuwatisha wanachama wote wa chama hicho wenye nia ya kugombea jimbo hilo mwaka huu. 


Viongozi hawa wameahidiwa zawadi nono endapo Kwagwilwa atarudi bungeni.


Akitoa taarifa kwa masikitiko makubwa, Mmoja wa rafiki wa karibu zaidi na Mbunge huyo  ambae ni Diwani katika Halmashauri ya Mji Handeni, amesema ni kweli Mbunge  amekuwa akimtumia Mwenyekiti wa CCM kuwatisha  viongozi wa kata ,matawi na wajumbe kwa ujumla.


Alisema kuwa, Mwenyekiti ndio mwenye kauli ya mwisho yaani mtu wa mwisho kusema katika chama ambapo Wajumbe wamekuwa wakimshangaa sana Mwenyekiti wao huyo kuwa mtu tofauti na alivyokuwa awali.

 

Mmoja wa wanachama wa CCM kutoka kata ya Chanika alisikika akisema  “Sisi wanachama wa CCM ambao tuna nia ya kugombea katika jimbo la Handeni mjini hatuna amani kabisa kwani Mwenyekiti wa CCM amekuwa akitumika na Mbunge vibaya kututisha endapo tutagombea na ameahidi kuwa atahakikisha tunafukuzwa ndani ya chama kabla ya muda wa uchaguzi ambapo hii ni kinyume na Katiba ya CCM inayomtaka kila mwachama anahaki ya kuchagua na kuchagulia” alisema mwana chama huyo.’’.


Mtoa taarifa ameendelea kudai kuwa, Mbunge amekuwa akimtumia Mwenyekiti huyo nyakati za usiku kuwafuata Wajumbe na kumwombea msamaha Mbunge huyo ambaye ameonyesha kutokuungwa mkono na watu wengi kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yake, kushindwa kutimiza ahadi zake pamoja na kujikweza baada ya kupewa nafasi hiyo.


Msemaji amesema pia alitumia nafasi hii kuwaomba Viongozi wa CCM ngazi ya Mkoa wa Tanga na Taifa kumuonya Mwenyekiti huyo kuacha kutumika kwa maslahi ya mtu mmoja na badala yake asimame katika nafasi yake na kuwaachia wanachama haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa.


“Yani huku kwetu Mwanaccm ukionekana humuungi mkono Mbunge ni kosa utatafutiwa kila aina ya fitina ili kuhakikisha kuwa unamuunga mkono Mh Mbunge au Mwenyekiti wa CCM wilaya akushughulikie hii sio haki kabisa


Alipotafutwa Mwenyekiti huyo kwa njia ya simu alisema kuwa, chama kinautaratibu wa kuwasemea viongozi waliopo madarakani kwani wametumwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi. 


Changogo alisema kuwa, viongozi wanapokuwa madarakani wao kama viongozi wa chama wanawajibu wa kuwasapoti na pale wanapomaliza muda wao na Binge kuvunjwa ndio inakuwa kikomo cha kutowasemea. 


"Siwatishi wanachama wengine wa CCM wenye nia ya kuchukua fomu pindi muda utakapofika kwani kufanya hivyo ni kukiuwa chama na Handeni kelele ni nyingi na nimeendelea kuvumilia kelele hizo" Alisema Changogo. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI