Header Ads Widget

MCHUNGAJI MSIGWA AWASHANGAA WANAOHAMA CHADEMA TUNDU LISSU AKIWA GEREZANI KUWA NI MATAPELI KISIASA


 Hawa wanaondoka Chadema ni matapeli wa kisiasa hivi wanasemaje Tundu Lissu anaharibu chama wakati uongozi wake hauna hata miezi mitatu pia yeye sasa yupo garezani anaharibu vipi chadema?waache uongo wao.

katika mahojiano na Matukio Daima Media mchungaji Peter Msigwa aliyewahi kuwa kiongozi wa Chadema na Sasa kuhamia CCM alisema hao ni waongo tu.

"Ninachopinga mimi hawa wanajitoa Chademasasa ni juu ya kutoa visingizio vya uongo ,mimi nilisema ukweli kuwa Mbowe amegeuza chama Saccos anakiua chadema leo mnashuhudia, ila hawa wanaotoka sasa ndio Team mbowe hii  tuliokuwa tukiwalalamikia waache uongo sasa"alisema Mch Msigwa 

Kuhusu yeye kugombea Ubunge

Kuwa pia anawashangaa sana wale wanaowaza kuwepo ndani ya chama ni lazima kuwa mbunge.

Mimi nawashangaa sana wanaowaza ubunge ama udiwani maisha sio lazima uwe kiongozi ndani ya chama unaweza kujiunga na chama na ukawa mwanachama wa kawaida,mimi nipo CCM ila si lazima kuwa mbunge siwezi sema sana kama nitagombea ama sigombei tutajenga daraja tukifika mtoni.

TAZAMA MAHOJIANO YOTE KWENYE LINK HII CHINI ⬇️⬇️⬇️⬇️

FULL MAHOJIANO NA MCHUNGAJI PETER MSIGWA BOFYA HAPA


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI