Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App Dodoma
KATIKA miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, Wizara imeendelea kuimarisha biashara ya nyama kwenda nje ya nchi, ambapo, mauzo yameongezeka kutoka tani 1,774 zenye thamani ya shilingi 9,867,000,000 kwa mwaka 2020/2021 na kufikia tani 13,745.38, zenye thamani ya shilingi 147,133,388,688 kwa mwaka 2024/2025.
Hivyo, kufanya jumla ya tani 40,635 zilizouzwa nje ya nchi zenye thamani ya shilingi 414,378,447,756 kwa muda wa miaka minne ya uongozi makini wa Jemedari wet na mwongoza njia Dkt.
Hayo ameyasema leo Mei 6 2025 jijini hapa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt, Ashatu Kijaji wakati akieleza mafanikio ya Miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Idara Maelezo Samia Suluhu Hassan.
Dkt , Kijaji amesema ongezeko hilo linatokana na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais kuongeza ushirikiano na fursa za kibiashara nje ya nchi .
"Hali hiyo Imesaidia kuongezeka kwa masoko ya nyama hadi kufikia nchi 12 ambazo ni Bahrain, Comoro, Hong Kong, Jordan, Kenya, Kuwait, Oman, Qatar, Rwanda, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Vietnam," Amesema Dkt,Kijaji.
Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita pia imeendelea kuboresha miundombinu kwa ajili ya mifugo nchini, ambapo, katika kipindi cha miaka minne, Serikali imejenga jumla ya Mabwawa 19 yenye thamani ya shilingi bilioni 10.69 kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji kwa mifugo, kutatua changamoto za jamii za wafugaji pamoja na kuimarisha afya ya mifugo nchini.
Ameeleza, Serikali imejenga na kukarabati minada ya mifugo 51 ya awali, upili na mipakani yenye thamani ya shilingi bilioni 18.26 kwa ajili ya kuboresha biashara ya mifugo na kupunguza matukio ya biashara haramu ya mifugo nje ya nchi kutokana na kukosekana kwa minada ya mifugo.
Pia, Serikaliimejenga vituo 10 vya kukusanyia maziwa, vyenye thamani ya shilingi bilioni 1.07 kwa ajili ya Wafugaji hususan wadogo kuwa na uhakika wa soko la maziwa kupitia.
Mwisho
0 Comments